Rozari Takatifu Ya Kibiblia
Ya Bikira Maria Mtakatifu

Rozari Takatifu Ya Kibiblia
Ya Bikira Maria Mtakatifu

Kwa Utatu Mtakatifu
Kwa Bikira Maria Malkia wa Rozari ya Pompei
Kwa Papa Yohana Paulo II

Utangulizi

Hii Rosari Takatifu ya Kibiblia ya Bikira Maria imeundwa na mafumbo saba, ya tafakari na sala, kwa siku saba za juma.

Ipo katika mpangilio na mtiririko wa kibiblia na pia mafumbo yake yanafuata mpangilio huo.

Kwa sababu hiyo, kwa kusali kila siku Rozari Takatifu tunaweza kutafakari Historia nzima ya Wokovu, inayofikia kilele chake Jumapili, siku ya ufufuko wa Kristo, siku ya Pasaka ya Bwana kwa ukamilifu wake.

Kwa hiyo kuingia mfumo wetu wa kibiblia katika kielelezo cha Bwana wetu Yesu Kristo na wa Mama yake Mtakatifu, mwenye heri (“µακαριοῦσίν με”: Lc 1,48) Bikira Maria, tutakuwa na mafumbo yafuatayo katika kila siku ya juma:

JUMATATU’ MAFUMBO YA UUMBAJI (“nafasi” au tafakari 6);
JUMANNE’ MAFUMBO YA NGUVU ZA MUNGU (“nafasi” au tafakari 6);
JUMATANO’ MAFUMBO YA FURAHA;
ALHAMISI’ MAFUMBO YA MWANGA;
IJUMAA’ MAFUMBO YA UCHUNGU;
JUMAMOSI MAFUMBO YA UKIMYA WA MUNGU (katika mtizamo wa Jumamosi kuu na ukimya wa Shabat);
JUMAPILI MAFUMBO YA UTUKUFU.

Hii inatuonyesha kwamba Rozari hii takatifu kamwe haina lengo la kuchungua nafasi:

  1. ya Rosari takatifu iliyowekwa na kutambuliwa rasmi na kanisa (Mafumbo ya Furaha - Mafumbo ya Mwanga - Mafumbo ya Uchungu - Mafumbo ya Utukufu);
  2. kujifunza, kutafakari na kusikiliza Neno la Mungu, Maandiko Matakatifu.

Hivyo sala na tafanari kwa njia ya Rosari hii takatifu vinataka kuwashauri na kwakumbusha bila kukoma katika kupenda na kutamani Maandiko Matakatifu, il kujua katika maisha yetu upendo wa Mungu ulivyo mkuu kwa ajili ya wokovu wa mwanadamu yote haya ni kama “mahangaiko” ya kimungu hili halimaanishi nyingine ila katika kuutafuta wokovu wa kweli wa mwanadamu. Wokovu unapatikana endapo tu mwanadamu atasema “NDIYO” kwa Mungu, yaani anajifungua jumla na bila woga, moyo wake asilia kwa Mungu.

Kwa Rosari hii takatifu tunampa Mungu utukufu na shukrani na tunampa nafasi halali, heshima halali Bikira Maria kulingana na ujumbe wa malaika wa Bwana alioutoa kwa mume wake Yosefu ambao una maana kwa kila mmoja wetu: “Usiogope kumchukua Maria awe mke wako, maana mimba yake ni kwa uweza wa Roho Mtakatifu” (Mt 1, 20).

Zaidi Ya Yote Kumbuka:

USIOGOPE! USIOGOPE! USIOGOPE!

BIKIRA MTAKATIFU ATAKUBEBA KWA SALAMA KABISA KUELEKEA KWA YESU!

Tunakushauri kujifunza masomo haya katika nyaraka au barua za kichungaji za Papa (S. Ioannes Paulus PP. II):


NAMNA YA KUISALI

  • Baada ya ishara ya msalaba, tunasali Atukuzwe Baba na zile sala pili za utangulizi, halafu tunalitangaza fumbo; inafuatiwa na Baba yetu (1), Salamu Maria (10) halafu Atukuzwe Baba… na zile sala pili za utangulizi. Halafu tunatangaza fumbo linalofuata na kuendelea kama ilivyoelezwa hapo juu.
  • kwa namna ya pekee wakati wa kusali “Baba yetu” na “Salamu Maria” (10) fanya akili (na moyo!) “kukimbilia” kutafakari juu ya fumbo lililotangazwa.

Hizi Ndizo Sala Pamoja Na Mafumbo Ya

Rozari Takatifu Ya Kibiblia
Ya Bikira Maria Mtakatifu:

Ishara Ya Msalaba: Kwa Jina la Baba na la Mwana na la Roho Mtakatifu. Amina!

Atukuzwe Baba, Mwana na Roho Mtakatifu, kama mwanzo na sasa na siku zote na milele. Amina.

Kubarikiwe siku zote kutungwa mimba bila dhambi ya asili kwa Maria Mtakatifu, Mama wa Mungu na Mama yetu.

Ee Yesu wangu, utusamee dhambi zetu, utukinge na moto wa milele, ongoza roho zote Mbinguni hasa za wale wanao hitaji zaidi Huruma yako.

[Tunatangaza Fumbo]

Baba yetu, uliye mbinguni Jina lako litukuzwe, ufalme wako ufike, utakalo lifanyike duniani kama mbinguni. Utupe leo mkate wetu wa kila siku, utusamehe makosa yetu, kama nasi tunavyowasamehe waliotukosea. Usitutie kishawishini bali utuopoe maovuni. Amina.

Salam Maria, umejaa neema, Bwana yu nawe, umebarikiwa kuliko wanawake wote na Yesu mzao wa tumbo lako amebarikiwa. Maria mtakatifu mama wa Mungu, utuombee sisi wakosefu sasa na saa ya kufa kwetu. Amina. (mara 10).

MAFUMBO YA UUMBAJI
(kwa Jumatatu)

  1. YHWH (Jahvè): Mungu Baba kwa njia ya Neno (ΛΟΓΟΣ - VERBUM), [“Awe!”], aumba mbingu na dunia na Roho Mtakatifu, ambaye tayari aliutangulia uumbaji kwa hekima yake alikuwa akielea juu ya maji yaliyo kuwa yameufunika uso wote wa nchi akivibariki viumbe.
  2. Mungu muumba mtu, mwanamme na mwanamke, wote aliwaumba kwa mfano na sura yake.
  3. Mungu mwahidia mwanmke baada ya dhambi ya asili kuwa kwa njia ya uzao wake, Masiha ataponda kichwa cha nyoka – adui wa mwanadamu.
  4. Melkisedeki, Mfalme na Kuhani, kinabii humpa Bwana mkate na divai kwa shukrani kwa ushindi wa Babu Mtakatifu Abrahamu (Mwa. 14, 18-20).
  5. Abrahamo aupokea ugeni, atambua na “kumkaribisha” Bwana, Utatu Mtakatifu karibu na mialoni ya Mamre (Mwa. 18, 1-15).
  6. Mungu amweka huru Isaka toka mauti kulingana na ahadi yake (“uzao wako utakuwa mwingi kuliko nyota za mbinguni na kuliko mchanga ulioko pwani ya bahari na kuimiliki miji ya adui zako” - Mwa. 22, 17) na kuimarisha Agano lake na Abrahamo (“na katika uzao wako mataifa yote ya dunia watajibarikia” – Mwa. 22, 18).

MAFUMBO YA NGUVU ZA MUNGU
(kwa Jumane)

  1. MUNGU, katika nafsi yake, awaokoa watu wake toka utumwani Misri na kuizindua Pasaka ya kwanza ya “umilele” (Kut. 12, 1-15).
  2. MUSA – mfano wa KRISTO - kwa Bakora aigawanya bahari ya Sham kwa ajili ya njia na uzima wa taifa teule na kuwaangamiza maadui wa Israeli kama isemavyo zaburi ya pili (Zab. 2, 8-9) ya mfalme masiha “uniombe, nami nitakupa mataifa kuwa urithi wako, na miisho ya dunia kuwa milki yako. Utawaponda kwa fimbo ya chuma, na kuwavunja kama chombo cha mfinyanzi.” na kama kisemavyo kitabu cha ufunuo wa Yohana (Ufu. 12, 5) “naye atamzaa mtoto wa kiume atakaye yatawala mataifa yote kwa fimbo ya chuma na mtoto alichukuliwa mara moja mbele ya Mungu na mbele ya kiti chake cha enzi”.
  3. NGUVU YA MUNGU, katika namna ya wingu ikatulia juu ya sanduku la agano Ambalo lilikuwa limewekwa katikati ya kambi ya wana wa Israeli ambalo katikati Yake kuna tabernakulo takatifu ambamo ndani yake Mungu ana kaa na ambamo taifa teule litapewa ishara tatu zilizokielezo cha Ekaristia Takatifu na Tabernakulo ya Ekaristia Takatifu: Vibao vya Sheria, yaani Neno lake (Verbum), “lililoandikwa kwa kidole cha Mungu” (hivyo kuja kwake moja kwa moja kama Mwana); Bakora ya Musa ni ishara nguvu aliyopewa na Mungu ambayo kwayo Musa aliigawanya ya Sham; Manna iliyoshuka toka mbinguni na ambayo huwashibisha wana wa Israeli huko jangwani.
  4. MUNGU amchagua Daudi na kumpaka mafuta kama Mfalme na Nabii juu ya watu wake Israeli na kuahidi Ufalme Milele kwa mwanae (katika uzao wake).
  5. JUDITA (Jd. 8-16), anayekata kichwa cha mfalme, adui wa wana wateule akiwaweka huru toka utumwani ni mfano wa MARIA aliyevaa jua na mwezi chini ya miguu yake na taji la nyota kumi na mbili ambayo huseta kichwa cha mfalme wa giza, “nyoka wa kale”, na kuwaweka huru wateule wa Kristo toka utumwa wa yule mwovu.
  6. NGUVU YA ROHO MTAKATIFU inajionyeshe pia katika ushahidi wa mzee Eleazaro (2 Mak. 6, 18-31), katika watakatifu ndugu saba wa Makabayo na Mama yao Mtakatifu (2 Mak. 7, 1-41), kwa kutokukubali kuiasi Sheria ya Mungu.

MAFUMBO YA FURAHA
(kwa Jumatano)

  1. Malaika mkuu Gabrieli ampasha habari Bikira Maria, na kwa “NDIYO” Yake, NAFSI YA PILI YA UTATU MTAKATIFU INAJIMWILISHA KATIKA TUMBO LAKE.
  2. Maria Mtakatifu amtembelea Mtakatifu Elizabeti.
  3. YESU ANAZALIEWA BETLEHEM.
  4. Yesu anatolewa Hekaluni ili aweze kutolewa sadaka kwa mungii Baba.
  5. Yesu anakutwa Hekaluni.

MAFUMBO YA MWANGA
(kwa Alhamisi)

  1. Yesu anabatizwa katika mto Jordan na Yohana Mbatizaji. – (Yesu anajipeleka kwa Yohana Mbatizaji ili aweze kubatizwa naye. Yeye habatizwi kwa ajili ya toba bali anapenda “kujishusha” zaidi na kujifanya mdhambi (ila bila dhambi) kati ya wadhambi. Mara baada ya kuingia majini mbingu zinafunguka, Roho Mtakatifu katika umbo la njiwa anatua juu yake na sauti ya Baba inatangaza toka juu mbinguni “Huyu ni Mwanangu mpendwa wangu niliyenipendezwa naye” - Mt. 3, 17).
  2. Yesu anafanya ishara ya kwanza katika maisha yake hadharani katika harusi ya Kana. - (Yesu alikuwa amealikwa pamoja na wanafunzi wake katika harusi ya Kana ya Galilaya. Wakiwa wameishiwa divai Yesu analetewa ombi na mama yake, anabadili maji kuwa divai. Injili inayoeleza tukio hilo inataarifu maneno ya mwisho ya mama Maria akituonya na kutualika daima kwamba «LOLOTE ATAKALOWAAMBIA, FANYENI !» - Yn. 2, 5).
  3. Yesu atangaza ujio wa ufalme wa Mungu. - (Yesu anatangaza kuwa ufalme wa Mbinguni u karibu na kwamba uko tayari kati yetu na kuthibitisha kuwa wataingia humo wale tu walioisafisha mioyo yao na kujinyenyekesha hata kujifanya «wadogo» kama mtoto).
  4. Yesu anabadilika sura katika utukufu wa Mungu juu ya mlima Tabor pamoja na Musa na Elia. - (Yesu anapanda mlima Tabor akiwa pamoja na Pietro, Yakobo na Yohana ili kusali. Mara kwa ghafla anabadilika sura katika utukufu wake wa kimungu anangara kuliko jua, karibu naye wanatokea Musa na Elia wakijadiliana kuhusu utume wake wa kimasiha kwa ajili ya wokovu, kwao yampasa aikabili Yerusalemu. Baba anatualika na anamtolea tena ushuhuda “Huyu ni Mwanangu mpendwa wangu ninayependezwa naye: MSIKILIZENI YEYE” - Lk. 9, 35).
  5. Yesu akiwa anaadhimisha Pasaka ya Kiebrania pamoja na Mitume wake katika ukumbi wa mlo wa jioni aliweka Ekaristia Takatifu. - (Juu ya mlima Sion, katika ukumbi wa Chakula cha Jioni, Yesu, akiwa anaadhimisha Pasaka ya Kiebrania pa moja na Mitume wake baada ya kuwa amewaosha miguu aliwapa mkate na divai akithibitisha ni mwili wake na damu yake vilivyotolewa kwa ajili ya wokovu wa watu wote. Ni adhimisho la Ekaristia Takatifu).

MAFUMBO YA UCHUNGU
(kwa Ijumaa)

  1. Yesu asali katika bustani ya Getsemani.
  2. Yesu anapigwa mijeredi.
  3. Yesu anavikwa taji la miiba na anahukumiwa kifo bila hatia.
  4. Yesu anapanda Calvari akibeba Msalaba.
  5. YESU AFA MSALABANI.

MAFUMBO YA UKIMYA WA MUNGU
UKIMYA UNAOFANYA KAZI YA MAPENDO NA YA HURUMA
(kwa Jumamosi)

  1. KRISTO, kati ya siku ya kufa na siku ya kufufuka kwake, siku ya “ukimya wa kimungu” aziweka huru roho za wenye haki na kuwaandalia nafasi mbinguni wao pamoja na wenye haki wengine watakao fuata.
  2. MARIA, kwa Upendo ya Kimama na Mama wa Kanisa zima, kwa licha ya Uchungu wa Kalvari, licha ya “upanga” uliompenya Moyo wake pale Kalvari anapata faraja, anatiwa moyo na kukaa siyo tu na Yohana bali hata Pietro na Mitume wengine wakiwa na uchungu, kuchanganyikiwa na usumbufu wa “kashfa” ya Msalaba.
  3. Huruma ya BABA kwa wanadamu haikatizwi na dhambi ya kumwaga damu na kumwua Mwanae-masiha Yesu Kristo, bali anaipokea kama sadaka jumla ya ukombozi wa wanadamu ambao Mungu aliwapenda, akawaumba kwa sura na mfano wake na kwa ajili ya wokovu wao akamtuma Mwanae wa pekee.
  4. MBEGU iliyoanguka chini kwenye udongo ikafa, maisha ya Kristo yaliyo tolewa sadaka na damu yake iliyo mwagika Kalvari vinachipusha leo hii toka katika ukimya wa kimungu maisha mapya na yasiyaharibika kwa wale wanaoupokea kulingana na mapenzi ya moyo wa Kristo.
  5. ROHO MTAKATIFU, katika kimya kikuu cha Jumamosi anaiandaa na kuifinyanga mioyo na akili za wampendao Mungu ili kulipokea tangazo la Ufufuko lisiloweza kuaminika kibinadamu kwa wale wampendao Mungu, kulipokea lisiloaminika (kibinadamu). Kwa tangazo la ufufuko, maana yeye, Yesu Kristo, “Hapo mwanzo kulikuwako Neno, naye Neno alikuwako kwa Mungu, naye Neno alikuwa Mungu. Huyo mwanzo alikuwako kwa Mungu: vyote vilifanyika kwa huyo, wala pasipo yeye hakikufanyika chochote kilichofanyika. Ndani yake ndimo ulimokuwa uzima, nao ule uzima ulikuwa nuru ya watu…Yeye ni Mwanzo na Mwisho, mwezayote …Yeye ni Mwana kondoo asiye na hatia milele yote yuko juu ya altare ya mbinguni na yeye tu mwenye kustahili kuchukua kitabu, kuvunja mihuri yake na kukifungua na kumkabidhi Baba kwa utukufu wa milele wa Mungu, wa malaika zake na watakatifu wake”.

MAFUMBO YA UTUKUFU
(kwa Jumapili)

  1. YESU ANAFUFUKA.
  2. YESU ANAPAA MBINGUNI.
  3. ROHO MTAKATIFU ANAWASHUKIA MITUME WAKIWA PAMOJA NA BIKIRA MARIA.
  4. Bikira Maria APALIZWA mbinguni.
  5. Bikira Maria AVIKWA TAJI Mbinguni Malkia wa Mbingu na Nchi.

SALAM, MALKIA!

Salam, Malkia! Mama mwenye huruma uzima tulizo matumaini yetu. Salam! Tunakusihi ugenini sisi wana wa Eva. Tunakulilia tukilalamika na kuhuzunika huku bondeni kwenye machozi. Haya basi mwombezi wetu utuangalie kwa macho yako ya huruma, Na mwisho wa ugeni huu utuonyeshe Yesu mzao mbarikiwa wa tumbo lako. Ee mpole, Ee mwema, Ee mpendelevu Bikira Maria.

LITANIA LAURETANA

Bwana utuhurumie! Bwana utuhurumie!

Kristo utuhurumie! Kristo utuhurumie!

Bwana utuhurumie! Bwana utuhurumie!

Kristo utusikie! Kristo utusikie!

Kristo utusikilize! Kristo utusikilize!

Baba wa mbinguni, Mungu, Utuhurumie!

Mwana mkombozi wa dunia, Mungu, Utuhurumie!

Roho Mtakatifu, Mungu, Utuhurumie!

Utatu Mtakatifu, Mungu, Utuhurumie!

Maria Mtakatifu, Utuombee.

Mzazi Mtakatifu wa Mungu,

Bikira wa Mabikira,

Mama wa Kristo,

Mama wa Upendo wa Kimungu,

Mama wa Neema ya Mungu,

Mama wa Rehema,

Mama wa Tumaini,

Mama mtakatifu sana,

Mama mwenye usafi wa moyo,

Bikira daima,

Mama usiye na doa,

Mama mpendelevu,

Mama mwenye kutamaniwa,

Mama wa sahuri jema,

Mama mfariji,

Mama wa Muumba,

Mama wa Mkombozi,

Mama wa Kanisa,

Mama wa Masikini,

Mama wa Mwisho,

Bikira uliyejaa hekima,

Bikira unayestahili heshima,

Bikira mwenye nguvu,

Bikira mwenye huruma,

Bikira mwaminifu,

Kioo cha utakatifu wa Mungu,

Kikao cha hekima,

Chemichemi ya furaha yetu,

Tabernakulo ya Roho Mtakatifu,

Tabernakulo inayong'ara,

Tabernakulo iliyowekwa wakfu kwa Mungu,

Tabernakulo ya Aliye Juu,

Waridi lenye fumbo,

Binti mteule wa Sion,

Mnara wa Daudi,

Mnara wa pembe,

Mnara imara,

Hekalu la dhahabu,

Sanduku la agano,

Mlango wa Mbinguni,

Nyota ya asubuhi,

Afya ya wagonjwa,

Kimbilio la wakosefu,

Mfariji wa wenye uchungu,

Msaada na Faraja ya Wahamiaji,

Msaada wa Wakristo,

Malkia wa Malaika,

Malkia wa Mababu,

Malkia wa Manabii,

Malkia wa Mitume,

Malkia wa Mashahidi,

Malkia wa Waungama Imani,

Malkia wa Mabikira,

Malkia wa Watakatifu wote,

Malkia uliyetungwa mimba pasipo dhambi ya asili,

Malkia uliyepalizwa Mbinguni,

Malkia wa Rozari Takatifu,

Malkia wa familia,

Malkia wa Amani,

Mama na Malkia wa Karmelo,

Mwana kondoo wa Mungu uondoaye dhambi za dunia, utusamee, Bwana.

Mwana kondoo wa Mungu uondoaye dhambi za dunia, utusikilize, Bwana.

Mwana kondoo wa Mungu uondoaye dhambi za dunia, utuhurumie, Bwana.

Utuombee Mzazi Mtakatifu wa Mungu, ili tuweze kustahili ahadi za Kristo.

Tunakuomba, Ee Bwana, utie Neema yako mioyoni mwetu ili sisi tuliojua kwa maelezo ya Malaika kwamba Mwanao Yesu Kristo aliyejifanya mtu, kwa Mateso na Msalaba wake, utuwezeshe kuufikia Utukufu wa Ufufuko. Kwa njia ya Kristo Bwana wetu. Amina.

Ishara ya Msalaba: Kwa Jina la Baba na la Mwana na la Roho Mtakatifu. Amina.


Arcidiocesi di Reggio Calabria-Bova - Nihil obstat, 12.2.2008

Santo Rosario Biblico della Beata Vergine Maria

Testo a cura di Carmelo Saraceno

Free counter

Realizzato da ITGO.it - Tutti i diritti riservati.